Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Emiliano Martinez: Kuna kombe jingine huko tuje kuchukua?

Emiliano Martinez Nm.jpeg Emiliano Martinez

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinda lango wa timu ya Taifa ya Argentina, Emiliano Martinez ameeleza kuwa hata bila Leonel Messi timu ina wachezaji 11 ambao wanaweza kupambana kama ambavyo walifanya kwenye mchezo wa fainali ya Copa America alipoumia nyota huyo.

Martinez anasema Leo Messi amechukua kila kombe aliloshiriki kwa ngazi ya Taifa na kwenye klabu amepata mafanikio makubwa na kama kuna jingine waambiwe wabebe kwa ajili yake.

"Kama Messi akiondoka kuna mashujaa 11 nyuma yake. Ni kiongozi wetu na tunachotakiwa kukifanya ni kupata ushindi kwa ajili ya timu."

"Kwenye fainali dhidi ya Colombia alilia lakini tukamfanya acheke mwishoni,.Amefanikiwa kwenye kila kitu. Kuna kingine kimebaki?," amesema Emi martinez Goalkeeper wa Aston Villa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live