Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Emerse Fae: Siamini kama tumefanikiwa

Emerse Fae Kocha Mkuu wa muda wa Ivory Coast, Emerse Fae

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa muda wa Ivory Coast, Emerse Fae, hakuweza kuelezea hisia zake kuu za kuwaongoza Tembo hao kubeba ubingwa wa Kombe la mataita ya Afrika ‘AFCON 2023’ nyumbani.

Fae amesema kuwa bado haamini kama kweli yeye ameiongoza Ivory Coast kubeba kombe hilo kwa mara yao ya tatu katika historia.

Ivory Coast ilitoka nyuma na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nigeria kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan Jumapili (Februari 11).

Akizungumza wakati huu wakiendelea a sherehe za ubingwa huo, Fae ambaye alichukua nafasi ya Kocha Mkuu Jean-Louis Gasset, amesema ni ngumu kuamini kwamba, walikaribia kutolewa na sasa wameshinda taji hilo.

“Bado naona vigumu kuamini. Tulipitia hisia zote. Ushindani huu utaashiria maisha yangu, hiyo ni hakika.

“Nilichukua mikoba ya timu tena wakati wa siku yangu ya kuzaliwa na nusura tutupwe nje, lakini mambo yaligeuka kutokana na bidii ya wachezaji hawa na sasa wamezawadiwa na kikubwa zaidi wametuza watu wetu waaminifu,” amesema kocha huyo

Fae pia alitwaa tuzo ya Kocha Bora wa Mashindano kwa kuonesha ustadi wa kuwaongoza “Tembo’ hao hadi kubeba kombe.

Chanzo: Dar24