Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eliud Kipchoge awa mgeni maalum Manchester United

Eliud Kipchoge.jpeg Eliud Kipchoge

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bingwa wa marathon Eliud Kipchoge kutoka Kenya alipewa hadhi ya kuwa mgeni maalum katika mechi kati ya Manchester United na Liverpool iliyofanyika Old Trafford.

Mshindi huyo wa mara mbili wa mbio za Olimpiki alipata wasaa wa kuzungumza na kocha Erik ten Hag wa Manchester United.

Akaunti rasmi ya mtandao wa kijamii ya X, ya Manchester ilisema ‘Shujaa yu kati yetu leo’.

Eliud Kipchoge ni kati ya wanariadha bora kuwahi kutokea ulimwenguni.

Ingawa hashikilii tena rekodi ya dunia kwa sasa, sifa yake kama mtu aliyebadilisha mtazamo wa mbio za marathon itaendelea kuishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live