Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

El Shenawy ndo basi tena AFCON

Mohamed El Shenawy Mohammed El Shenawy

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nuksi imeendelea kuiandama kambi ya timu ya taifa ya Misri inayoshiriki fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) zinazoendelea huko Ivory Coast, baada ya kipa wake chaguo la kwanza, Mohamed El Shenawy kupata majeraha yatakayomfanya akose mechi zote zilizobaki za mashindano hayo.

Shenawy amepata jeraha la bega katika dakika za nyongeza za mchezo baina ya Misri na Cape Verde uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 ambapo alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Mohamed Abou Gabal 'Gabanski'.

Jopo la matabibu wa Misri limetoa ripoti ya awali kuwa mchezaji huyo amepata tatizo la mfupa wa bega kuhama, hivyo kwa tathmini ya haraka, atahitajika kuwa nje ya uwanja kwa muda usiopungua miezi miwili.

Majeraha ya Shenawy yametokea katika muda usiozidi wiki moja tangu nyota wa Misri, Mohamed Salah alipopata maumivu ya misuli ambayo yatamuweka nje kwa wiki mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live