Baada ya michezo 33 ya kuitumikia klabu ya Al Ain akifunga mabao 15 na kutoa assists 18, Januari 2019 Hussein El Shahat alijiunga na Al Ahly kwa ada ya usajili ya Dola za kimarekani Milioni 5 (Kama bilioni 12.5 kwa viwango vya Leo vya kubadilisha fedha) ambazo Ahly walilipa kwa mikupuo miwili.
Huyu ndiye mchezaji wa bei ghali zaidi kuwahi kununuliwa barani Afrika kwenye dirisha la usajili akifuatiwa na Marcel Allende wa klabu ya Mamelodi Sundowns aliyesajiliwa kwa dau la Randi za Afrika Kusini Milioni 51 ambazo ni kama Bilioni 6.84 za Kitanzania.
Kumbuka huu ni usajili wa dirisha dogo kwa nchi zinazotumia kalenda ya mashindano ya FIFA na ulikuwa ni usajili wa 5 kwa Ahly kwenye majira hayo!
Rais wa Al Ahly Mahmoud El Khatib ndiye aliyesimamia usajili huu kuhakikisha unakamilika na tangu ameingia Ahly, Shahat ni miongoni mwa wachezaji tegemeo na ameshashinda CAFCL mara 3.
Hussein Ali El Shahat Ali Hassan mwenye urefu wa futi 5.7 na uzito wa KG 68 anasifika kwa uwezo mzuri wa kutunza mpira mguuni, kasi na maamuzi ya haraka ingali msimu huu hajarudi kwenye ubora wake.