Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eh! Dabo aichezea Yanga akili kubwa

Dg Bangala Fei Toto Eh! Dabo aichezea Yanga akili kubwa

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Azam juzi kilikuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Bandari kutoka nchini Kenya huku kocha mkuu wa timu hiyo, Youssouph Dabo akitumia akili kubwa kabla ya kukutana na Yanga Agosti 9 kwenye Ngao ya Jamii.

Timu hizo zitakutana katika mchezo huo mkali unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka kutokana na usajili wa mastaa Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Yannick Bangala walioondoka Yanga na kutimkia Azam msimu huu.

Katika mchezo huo na Bandari, Dabo aliwaambia viongozi wa timu hiyo wasiruhusu mashabiki kuingia uwanjani au kuonyeshwa kwenye televisheni kwa lengo la kutotaka mbinu anazotumia kuvuja haraka mbele ya wapinzani wao.

“Kocha amekuwa makini sana katika kipindi hiki cha maandalizi ya mchezo wetu na Yanga kwa sababu hataki iwe rahisi mbinu anazotumia kutufundishia zivuje haraka kabla ya mashindano,” alisema mmoja wa wachezaji wa timu hiyo.

Awali, wakati anazungumza na Mwanaspoti, Dabo alisema licha ya kufurahishwa na morali ya wachezaji ila lengo la michezo hii mingi ya kirafiki ni kutaka kutengeneza muunganiko wa kiuchezaji na mbinu kabla ya mashindano.

Azam iliweka kambi ya wiki tatu nchini Tunisia ambapo ilicheza michezo minne ya kirafiki ikishinda 3-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan na (2-1) na US Monastri huku ikipoteza pia (3-0) na Esperance, (3-1) na Stade Tunisien.

Azam inakutana na Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) msimu uliomalizika kwenye uwanja huo huo pia.

Chanzo: Mwanaspoti