Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edward Manyama aaga Azam FC

Edward Manyamaaaa Manyama

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam wameachana na beki wao kiraka wa kati, Edward Charles Manyama baada ya mkataba wake kutamatika.

Manyama ameaga rasmi kwenye Klabu ya Azam FC wakati akiwa kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan.

"Bye bye Azam Fc bye bye Chamazi ni ngumu sana ila ni wakati sahihi wa mimi kuondoka kwenye Familia ya Azam Fc.

"Nimeshindwa hata kuandika kwa sababu ya upendo wenu Wafanyakazi, Wachezaji, Benchi la ufundi, Viongozi, Mashabiki, nawatakia Maisha yenye furaha malengo tele mungu awabariki sana sana," ameandika beki huyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Manyama alijiunga na Azam Fc akitokea Namungo Fc mwaka 2021. Pia, beki huyo amewahi kuvitumikia vilabu vya JKT Ruvu Stars, Yanga sc, Ruvu Shooting, Namungo FC pamoja na Azam Fc.

Anaitwa Edward Manyama

Alizaliwa 2 Aprili, 1994

Ana umri miaka 30

Anacheza nafasi ya beki wa kati/kushoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live