Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eduardo Mendy aweka ngumu Chelsea

Edouard Mendy Chelsea F365 5 Mlinda mlango wa Chelsea, Edouardo Mendy

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinda mlango wa Chelsea Edouardo Mendy amekataa nyongeza ya mkataba mpya wa miaka 6 wa kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya Stamford Bridge kwa sababu anaamini klabu hiyo haimuoneshi heshima anayostahili kwenye mshahara.

Kwa mujibu wa The Sun Chelsea ilitaka kumuongeza miaka 6 zaidi katika mkataba wake wa sasa ambao utatamatika baada ya miaka miwili na nusu lakini Msenegal huyo amegoma anataka mshahara zaidi.

Inadaiwa Mendy (30) kwa sasa analipwa pauni laki moja lakini hataki kuendelea kulipwa kiasi hicho na anataka kulipwa mshahara unaokaribia ule wa nyanda mwenzake Kepa Arrizabalaga ambaye analipwa karibu mara mbili ya Mendy sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live