Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eduardo Camavinga ashika pabaya Real Madrid

Camavinga Eduardo Camavinga

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: Dar24

Mabingwa wa Soka Barani Ulaya Real Madrid, wanatajwa kuwa kwenye mpango wa kumpa mkataba mrefu kiungo kutoka nchini Ufaransa Eduardo Camavinga ambao utamuwezesha kulipwa mshahara mnono.

Camavinga mwenye umri wa miaka 20, amekuwa moja kati ya nyota muhimu anayeendelea kuandaliwa katika eneo la kiungo kikosini hapo.

Kiungo huyo amekuwa msaada klabuni hapo akiwa na msimu wake wa pili ndani ya Real Madrid aliyojiunga nayo akitokea Rennes ya nchini kwao Ufaransa.

Tayari akiwa hapo, ameshinda taji la La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya, UEFA Super Cup, Klabu Bingwa Dunia na Spanish Super Cup.

Madrid imejipanga kumpatia mkataba mpya ambao mshahara wake utaongezwa maradufu.

Camavinga inaelezwa kuwa ofa ya mkataba wake mpya inaweza kuwa mwezi ujao, huku timu ikijipanga kuboresha maslahi yake.

Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez anadaiwa kumuhususdu sana Camavinga kutokana na ubora wake katika eneo la kiungo.

Chanzo: Dar24