Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe awafunda wanachuo Tengeru

Chuga Pic Data Mwandishi wa Habari na Mchambuzi, Edo Kumwembe

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mchambuzi nguli wa michezo nchini Tanzania na Mwanahabari, Edo Kumwembe amewataka wanachuo  wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (CDTI) kuwa na kipaumbele cha elimu pamoja na michezo kwani vyote vinaenda sambamba katika kukuza na kuinua vipaji.

Ametoa rai hiyo wakati akizungumza katika uzinduzi wa Bonanza la michezo kwa mashabiki wa Simba na Yanga chuoni hapo, kwa ajili ya kuwakaribisha wanachuo wapya na kutoa motisha kwao kupenda michezo.

Amesema kuwa, swala la michezo vyuoni ni la muhimu Sana kwani linatoa chachu kwa jamii hiyo kuweza kuinua vipaji vyao kwani wachezaji bora  wengi wametokea vyuoni ,huku akiwataka kutoa kipaumbele katika elimu kwanza kwani ndio akiba kubwa .

"Wachezaji wengi  wakubwa mnaowaona wametokea kwenye vyuo kama hivi unakuta mtu alikuwa anasomea taaluma nyingine , lakini pia kupitia michezo vyuoni anaweza kuinua na kuendeleza kipaji chake na kuweza kufika mbali kama walivyo wachezaji wengine wakubwa huku akimtolea mfano mchezaji wa Simba Theadeo Lwanga ambaye yeye kitaalamu ni Mhandisi lakini anasakata kabumbu."amesema Edo.

Hata hivyo Edo ameeleza kuvutiwa na vipaji vya soka katika bonanza la mashabiki wa Simba na Yanga ambalo limehusisha wanafunzi na waalimu wa chuo hicho na kuvitaka vilabu mbalimbali vya mpira kuvitupia jicho.

Naye Mkuu wa Taasisi hiyo ya maendeleo ya jamii Tengeru,Dokta Bakari George amesema kuwa, lengo kubwa la kuandaa Bonanza hilo la michezo katika mpira wa miguu na mpira wa kikapu kwa wasichana  ni kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa Kwanza zaidi ya elfu moja ambao wamesharipoti chuoni hapo.

Amesema kuwa, kuwa kufanya hivyo itaweza kuleta chachu kwao kupenda michezo na hata kuendeleza vipaji kwani wamekuwa na utaratibu huo kila mwaka huku mafanikio yakiwa makubwa sana.

"Katika bonanza hili  timu hizi zilizoshiriki pande zote ni timu ya   Simba na Yanga kwa wanafunzi wa vyuo pamoja na waalimu pia ,na kupitia mabonanza haya mwisho wa siku ni kutaka kuendeleza na kuinua vipaji mbalimbali nje ya taaluma zao  kwani michezo nayo ina umuhimu wake ," amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa Bonanza hilo, Elifadhili Mpehongwa amesema kuwa,wamekuwa wakifanya Bonanza hilo kila mwaka ambapo lina lengo kubwa la kuhamasisha michezo kwa wanafunzi hao na kuweza kukuza vipaji vyao nje ya taaluma.

"Pamoja na kuwa wanafunzi hawa wamekuja na malengo yao ya kusomea taaluma mbalimbali ila katika hayo pia wataweza kukuza na kuendeleza vipaji vyao kupitia michezo kwani nje ya taaluma zao pia wanaweza kuendeleza vipaji vyao na vikawasaidia mbeleni," amesema Mpehongwa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz