Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe awachana wanaosema Yanga iliweka kiingilio kikubwa

Mashabiki Yanga Kwa Mkapa Edo Kumwembe awachana wanaosema Yanga iliweka kiingilio kikubwa

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Edo Kumwembe amewaponda baadhi ya wachambuzi na mashabiki wa soka ambao wamesema chanzo cha Yanga SC kushindwa kuujaza Uwanja wa Mkapa katika Tamasha lao Siku ya Mwananchi ni kiingilio cha Tsh 10,000 kuwa kikubwa.

Tamasha hilo lilifanyika Jumamosi iliyopita ambapo Yanga walitangaza wachezaji wao watakaokuwa nao kuelekea msimu mpya huku wakicheza mechi ya kirafiki na kaizer Chiefs ya Afrika Kuzini ambapo yanga walishinda kwa bao 1-0.

Akizungumzia hilo, Edo amesema; "Umekaa na mtu baa, amekunywa bia 21, ubavu wa mbuzi na kaita demu wake. Bado na yeye analalamika kwamba 'Elfu kumi nyingi kuingia uwanjani'. Yes kuna watu elfu kumi nyingi sana lakini kuna watu wanaiga tu kusema elfu kumi nyingi kwa sababu hawajazoea kulipa au hawajazoea ughali wa mpira.

"Kuna kundi kubwa la wenye uwezo wa kulipa elfu kumi hawaendi uwanjani wakitumia kisingizio cha sh elfu kumi wakati ni wababe wa starehe sehemu nyingine. Tanzania ni miongoni mwa nchi chache ambazo mpira kulipia ni bei rahisi. Yaani anakuja Mahrez unamtazama kwa dola moja tu (sh elfu tatu).

"Kamuulize Injiani aliteseka kumpata Max, Skudu, na wengineo kwa sh ngapi. Hadi dirisha lifungwe ukute wametumia sh milioni 600 kusajili, achana kuvunja mikataba. Simba imetumia sh ngapi kusajili? Kuweka kambi Uturuki? Hata hivyo tunataka kiingilio kiwe dola moja tu kwa ajili ya kufurahisha mashabiki.

"Tumekaa tunasubiri akina Miquissone tuwaone kwa dola moja tu wakati timu imetumia sh milioni 200 kumrudisha nchini. Yeye peke yake achilia mbali akina Onana. Starehe nyingine tunazifanya kwa bei ghali lakini mpira tunautaka uwe rahisi sana. Nchi ya kijamaa sio?," amesema Edo Kumwembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: