Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe ataja sababu presha ya mashabiki wa Simba

Edo Kumwembe Wasafi Edo Kumwembe ataja sababu presha ya mashabiki wa Simba

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Edo Kumwembe amesema kinachowafanya mashabiki wa Simba wawe na presha kubwa ni kwa sababu, ligi ya Bongo hakuna timu inayoweza kukusaidia kazi timu kubwa endapo utapoteza michezo kadhaa.

Amesema, utofauti wa Simba na Yanga kwa sasa ni alama 5 tu tena Simba akiwa na mchezo mkononi lakini mashabiki wanapagawa kwa sababu wanaamini ni ngumu mpinzani wao Yanga kupoteza tena mpaka msimu unaisha.

"Kuna presha kubwa sana katika soka letu, hasa kwa hawa Simba na Yanga....kuna sababu nyingi lakini zaidi ni kwamba nchi imegawanyika katika pande mbili kwao. Kwa mfano, Simba imeachwa pointi tano tu na Yanga huku ikiwa na mechi mkononi lakini inaonekana kuna crisis kubwa Simba.

"Bado Simba ipo makundi CL. Huku katika Ligi issue ni kwamba ukipitwa inaonekana umepitwa kwa sababu hakuna watu wa maana kukusaidia kazi kama Ulaya ambako Brentford anaweza kumchapa Man City....yaani huku kwetu ukiachwa katika msimamo ndo inaonekana umeachwa mazima," alisema Edo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live