Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe amtonya Gamondi

Gamondi 547 Edo Kumwembe amtonya Gamondi

Tue, 9 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wanatamani Aziz Ki, Chama, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli wote waanze kwa pamoja na mbele yao asimame Prince Dube. Miguel Gamondi anaweza kujikuta akifanya kosa kwa kuwaanzisha wote kwa pamoja.

Wakati mwingine ukiwaanzisha mastaa wote kwa pamoja timu inakosa uwiano. Wachezaji hawa wenye vipaji wanapaswa kulindwa na wachezaji wenye kariba ya ukabaji na matumizi mazuri ya nguvu.

Real Madrid waliwahi kutengeneza timu ya ndotoni kama hii wakaishia kuwa kichekesho kutokana na ukosefu wa uwiano kati ya ukabaji na ushambuliaji.

Florentino Perez kwa pamoja aliwachukua David Beckham, Zinedine Zidane, Luis Figo, Raul Gonzalez na Ronaldo de Lima akataka wote wacheze kwa pamoja. Waliitwa Galacticos. Waliishia kuambulia vichapo vya mara kwa mara kwa sababu timu ilikosa wakabaji.

Mbaya zaidi akamuuza Claude Makelele kwenda Chelsea baada ya kugoma kumuongezea mshahara. Perez alikuwa na sababu zake za kibiashara zaidi kufanya hivyo ili mauzo ya jezi yaongezeke lakini pia mashabiki waendelee kununua tiketi kwa wingi ili kuiona timu hii ya ndotoni ikisakata soka.

Hata hivyo, mpango mzima ulishindikana kutokana na wachezaji wengi mastaa kutokuwa wakabaji sana uwanjani kitu ambacho kwa kiasi kikubwa kiliwagharimu walinzi.

Gamondi kama kocha mwenye akili timamu sio lazima awaanzishe wote kwa pamoja hasa katika mechi kubwa ambazo Yanga nao watalazimika kukaba. Kinachopaswa kufanyika ni wengine kuanzia nje kwa ajili ya kuingiza wachezaji watakaoweza kufanya kazi chafu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live