Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe: Tumeamua kumfanya Onyango mbuzi wa kafara

Edo X Onyango Edo Kumwembe: Tumeamua kumfanya Onyango mbuzi wa kafara

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama kuna mlinzi angekuwa anamsaidia Onyango kwa karibu (compactness) si ajabu asingeona umuhimu wa kumgusa mpinzani au kuendelea kusuguana naye katika mwili.

Wenzetu katika mazingira yale, wakati Onyango anaachwa kwa ujanja na mpinzani tayari kungekuwa na mchezaji mwingine wa Simba amejitokeza kumsaidia Onyango.

Na sasa kelele zimekuwa nyingi kuhusu Onyango. Kitu ambacho siamini ni kwamba mchezaji anaweza kwisha ghafla. Mfano tu ni kwamba msimu uliopita Onyango alikuwa bora, halafu ghafla sasa hivi amekwisha. Kinachotokea kwa sasa ndicho ambacho kitammaliza kabisa Onyango. Hizi shutuma ndizo ambazo zitamfanya aanze kutojiamini.

Wenzetu huwa wanamnyanyua mchezaji kutoka hapa alipo ili arudishe ubora wake. Sisi huwa tunamzamisha zaidi kwa kuendelea kumshutumu kuwa “Ni mzee atupishe” na maneno mengine ya kejeli. Kuna mambo mawili.

Ama Simba iende sokoni na kumnunua beki mwingine ambaye atakuwa kama bahati nasibu tu. Anaweza kuja akafanya makosa mengi kuliko Onyango. Lakini jambo la pili wanaloweza kufanya ni kumtia moyo Onyango arudi katika kujiamini na ubora wake ili waokoe pesa na muda.

Kwa sasa naona tunataka kumtoa mchezoni kama ilivyo kawaida yetu. Sio jambo jema sana. Mchezaji haishi ghafla. Huwa anaisha taratibu. Nasimama kumtetea mpaka pale atakapozidisha makosa tena na tena. Kwa sasa bado ana nafasi ya kutamba Simba. Kama tunadhani hafai basi tumpange Mohamed Ouattara. Mbona hachezi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live