Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe: Timu zetu kushinda nje sio dili tena

Edo Kumwembe Kushinda Ugenini Edo Kumwembe: Timu zetu kushinda nje sio dili tena

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwandishi na mchambuzi wa Soka nchini Edo Kumwembe amesema kuwa kwa sasa kitendo cha Timu zetu kushinda michezo yake ya ugenini kwa Mashindano ya CAF sio kitu cha kushangaza wala kujipa sifa bali mipango yetu iwe katika namna ya kunyakua mataji ama kufika hatua za juu zaidi ambazo hatujawahi zifikia.

Edo ameongea maneno hayo huku akitolea mifano ushindi waliopata Timu za Simba na Yanga kwa nyakati tofauti katika michezo yao ya michuano ya CAF msimu huu;

“Juzi Simba waliichapa Vipers ugenini. Yanga pia waliichapa Club Africain kwake. Simba pia walitembeza kichapo kwa Primeira de Agosto kwake Luanda. Inaonekana kama vile klabu zetu zimeanza kuzoea kushinda nje. Ukweli ni kwamba zamani hatukuzoea hivyo.”

Simba inashiriki Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Yanga inashiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live