Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe: Simba haishindi kwa mbinu za Robertinho

Edo Robertinho Edo Kumwembe amsagia kunguni Kocha Robertinho

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba ikiibuka na ushindi wa pili mfululizo michezo ya hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, bado kuna watu hawaoni timu hiyo ikifanya yale ambayo imekuwa ikiyafanya katika michezo yake ya michuano iliyopita.

Wachambuzi wengi na mashabiki wanasema Simba inashinda lakini haichezi mpira mzuri, wa mipango kama ilivyokuwa hapo awali.

Miongoni mwa wachambuzi waliotoa mitazamo yao ni Edo Kumwembe ambae yeye amekwenda mbali na kudai kuwa pengine Timu imemshinda.

Akizungumza Edo anasema;

"Kila siku namsikia Robertinho akiomba kupewa mda lakini hivi sasa ni Mwezi wa tatu akiwa Simba ila hatuoni mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika eneo lolote lile.Hata ukiangalia Ushindi wa jana ulipatikana kwa sababu ya morali ya wachezaji tu na sio ubora wake"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live