Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe: Nimefurahi Yanga kufungwa

Edo Kumwembe Wasafi Edo Kumwembe

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Mchezo wa Watani wa jadi kati ya Simba na Yanga ukitamatika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kufuta uteja mbele ya Yanga wa kutoshinda kwa miaka 3.

Mchambuzi wa Michezo kutoka kituo cha Wasafi FM, Edo Kumwembe yeye anasema amefurahi Yanga kupoteza mchezo huo.

Akifafanua Edo anasema;

"Mimi nimefurahi Yanga kufungwa, naamini Yanga angeshinda isingekuwa story kubwa kama ilivyo sasa kwa Simba kwa sababu wameifunga sana Simba siku za hivi karibuni.. Simba kushinda kutaongeza mvuto wa derby, Inawezekana tukaishuhudia derby nyingine ya Simba na Yanga msimu huu kwenye Kombe la (FA)"

"Yanga hawakuwa wamejiandaa na mechi, waliona kama wameshashinda mechi kiurahisi na sio tu kwamba watashinda, watafunga mabao mengi. Simba walikuwa kimya wiki nzima, kuna jambo lao walikuwa wanaliwinda"

“Kwanza nimemshangaa sana Kocha Nabi kumlalamikia mwamuzi, Hadi Half time Yanga ilibidi wapigwe bao 4.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live