Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe: Mexime amemkosea Benchikha, amembagua kwa rangi

Edo Kumwembe: Mexime Amemkosea Benchikha, Amembagua Kwa Rangi Edo Kumwembe: Mexime amemkosea Benchikha, amembagua kwa rangi

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Bongo Edo Kumwembe, amekosoa kitendo cha Kocha wa Kagera Sugar kuonesha kile alichokiita 'ubaguzi wa rangi' kwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdallek Benchikha.

Amesema kwamba, kwa namna yoyote, Mexime alitakiwa kumheshimu Benchikha na kutotaja suala la rangi katika mazungumzo yake.

"Jana nimesikitika sana....wakati rafiki yangu Mecky Mexime akimpuuza kocha wa Simba, Benchikha kwa kudai;

"Basi tu kwa sababu yeye mweupe na anavaa kofia lakini mbinu zetu ni zile zile tu".....ameongea na watu wameona kawaida.

Leo Simba akimfunga Kagera halafu Benchikha akasema;

"Kocha wao hana uwezo kwanza ni mweusi na ana upara"....wabongo wote tutakuja juu kwamba Benchikha ni mbaguzi. Tatizo letu tunadhani ubaguzi ni mtu mweupe kumbagua mweusi kwa rangi yake.

Jana Benchikha kabaguliwa kwa muktadha wa alichoongea Mecky. Kama Mecky angemaanisha kuwa Benchikha anabebwa kutokana na kuwa kocha wa kigeni, hapo sawa, lakini issue sio weupe.

Lakini hata kwa muktadha wa mafanikio tujifunze kwa waliotuzidi. Benchikha ana mataji mengi tena akichukua katika nchi ambayo imetuacha mbali kisoka. Last season tu amechukua confederation," aliandika Edo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live