Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe: Kwa nini Onyango asicheze Dabi, Yanga sio Raja

Edo X Onyango Edo Kumwembe: Kwa nini Onyango asicheze, Yanga sio Raja

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wengi wakionekana kuwa na mashaka na kiwango cha Beki Mkenya Joash Onyango kuelekea mchezo wa Dabi ya Kariakoo Aprili 16.

Mchambuzi kutoka Wasafi Fm Edo Kumwembe amesema makosa aliyoyafanya Onyango kwenye mechi za kimataifa hayawezi kumfanya akose nafasi kwenye mechi ya Kariakoo Derby kwa sababu makosa hayo aliyafanya wakati akiwa kwenye Timu zenye kiwango kikubwa.

“Onyango tumuache kwenye hayo makosa kwa sababu yalikuwa ni kwenye Top Level ni Against Raja mjue, Raja sio Yanga asikudanyanye mtu, wanaweza kuwa wazuri lakini Raja sio yanga.

“Kwani Onyango si anacheza kila siku hayo makosa kafanya? Onyango kamdhibiti Mayele mara ngapi ?, si tulikuwa tunamsifu hapa kwa kumdhibiti Mayele,”

Simba wataikaribisha Yanga katika Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili mchezo wa mzunguko wa pili Ligi Kuu ya NBC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live