Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe: GSM mpeni Feisal pesa inayoeleweka

Edo Fei Toto Edo Kumwembe amshauri Feisal kiaina

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuanza msimu kwa kasi ya hali ya juu, Kiungo wa Kitanzania kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum ameanza kupigiwa debe apewe Mkataba unaoendana na na kiwango anachoonesha.

Feisal ambae mara kadhaa amekuwa akiwapa Yanga matokeo kwa magoli yake ya kusisimua, Jana Disemba 4 katika Uwanja wa Mkapa kwa mara nyingine aliwapa Yanga alama tatu muhimu kwa bao lake la dakika za lala salama.

Sasa Mwandishi wa habari mwandamizi na mchambuzi wa Soka Edo Kumwembe kiaina amemshauri Feisal kudai maslahi zaidi katika mikataba yake na Yanga.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Edo ameandika;

“GSM wakishauza furniture sijui magodoro....mwishoni mwa msimu wampe Feisal hela inayoeleweka.

“Huwa nawashangaa akina Mpenja wanapomuita Feisal kama 'Zanzibar Finest'....

“Fei kwa sasa ndiye mchezaji bora zaidi wa local eneo la kiungo kwenda mbele hapa kwetu achilia mbali mambo ya Zanzibar...one of the very best....uzuri ndani na nje ya uwanja anakuwa na furaha...."

Mkataba wa sasa wa Feisal unamalizika 2o24 huku kukiwa na tetesi za Matajiri wa Azam kumnyatia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live