Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edna Lema: Wachezaji wa kike msijiweke kiume

Dfsg Edna Lema: Wachezaji wa kike msijiweke kiume

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha msaidizi wa Biashara United, Edna Lema 'Mourinho' amewataka baadhi ya wachezaji wa kike nchini kujikubali na kujiweka kama wanawake na isiwe katika mwezi wa mfungo wa Ramadhan pekee.

Kabla ya kujiunga na Biashara inayoshiriki Championship, Edna alizifundisha timu za taifa za wanawake na pia Yanga Princess.

Akizungumza na Mwanaspoti, Edna alisema aliona picha ya mchezaji mmoja akiwa amevaa kwa stara na kubeba picha halisi ya mwanamke katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi wa Ramadhan na kuwataka wajiweke hivyo siku zote.

Alisema kwa wachezaji kunahitajika kupewa semina ya mara kwa mara ya kusakata kabumbu wakikubali wanawake watakaokuja kuwa na familia baadaye.

"Unaweza kucheza na muonekano wako kama mwanamke na watu wakakuelewa, tunapaswa kuishi maisha halisi kama watoto wa kike na sio kuchagua siku 30 za mwezi mtukufu ndio tunabadilika ikiisha basi tunarudi kiuwanaume, mbona wanavutia tu wakiwa kwenye mionekano yao ya kike na uwezo wao hauwezi kuathiriwa na mavazi," alisema na kuongeza:

"Tunapaswa kukumbushana kwamba hatuchezi mpira milele kuna wakati tunapaswa kujenga familia zetu, tuache miguu yetu izungumze na tubaki kwenye uhalisia wetu na tusichukulie kama jinsi yetu inatukaba kutimiza ndoto zetu."

Hilo linakuja baada ya kuona kuna wimbi kubwa la baadhi ya wachezaji wa kike nchini wakijiweka mionekano ya kiume, jambo ambalo linaweza kuwatisha wazazi hadi wawawekee vikwazo mabinti zao kwenda kucheza soka kwa kuhofia watageukia maisha ya aina hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti