Kocha mwenye mbwembwe nyingi kwenye soka la wanawake Edna Lema (Mourinho) amesema kuwa yeye hana presha ya kupata kazi kwa sasa kwa kuwa ana amini kupitia taaluma yake.
Mourinho ambaye aliachana na Yanga Princess mwanzoni mwa msimu wa ligi iliyopita alisema, kama kocha kuna wakati ukosa kazi na hiyo imemkuta yeye na hana wasiwasi.
Mourinho alisema kuwa hata kwenye timu za taifa ambazo uwa anasimama kama kocha msaidizi hayupo tena: “Sipo kwenye timu yoyote kwa sasa.
“Lakini sina presha na maisha yangu yanasonga vizuri tu. Kuna wakati lazima ukubali kila kitu na kusubiri wakati sahihi ufike. Kocha kutokuwa na kazi ni kawaida sana.”