Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edinson Cavani kuwakosa Atletico Madrid

Edinson Cavani.jpeg?fit=736%2C485&ssl=1 Mshambuliaji wa Man United, Edson Cavani

Wed, 23 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Edinson Cavani hatasafiri na timu kwenda Hispania kwenye mchezo wa 16 bora kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya klabu ya Atletico Madrid.

Edinson Cavani amekosa michezo mitatu kutokana na majeraha ya groin, kocha wa muda Rangnick amethibitisha kwamba mchezaji huyo mwenye miaka 35 hataweza kusafiri na timu kwenda madrid, alipohojiwa na waandishi kuhusu Cavani kuwepo kwenye kikosi kitachosafiri alijibu.

“Edi hata kuwepo kwenye sehemu ya watu watakao safiri, hajafanya mazoezi ya pamoja na timu kwa wiki kadhaa na hata kuwepo kwenye safari.”

alipoulizwa kuwa lini anatarajia cavani kurudi kwenye kikosi chake aliongezea, “anatatizo la groin, na kadri atavyojiskia kutokuwa sawa kukimmbia hatajumuishwa, haileti maana kumrudisha mazoezuni na kumlazimisha kufanya mazoezi, nadhani anauzoefu wa kutosha wa kujua yeyemwenye ikiwa yupo sawa kurudi tena.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live