Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ederson apambana awawahi Arsenal

Skysports Man City Ederson 5602425 Ederson apambana awawahi Arsenal

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa Ederson atapambana na hali yake kuwa fiti ili kuwamo kwenye mechi muhimu ya Manchester City watakayokipiga na Arsenal mwishoni mwa mwezi huu.

Kipa huyo Mbrazili aliumia paja kwenye mechi ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Liverpool, Jumapili iliyopita, lakini sasa anapambana ili awe fiti kuwakabili wapinzani wao wengine kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Awali kwenye vipimo alivyofanyiwa Jumatatu zilionyesha kipa huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kuanzia wiki tatu hadi nne. Hiyo ina maana, atakuwa sawa kucheza kwenye mechi ya Arsenal itakayofanyika Jumapili Pasaka, Machi 31, na ile mechi ya Aston Villa itakayofanyika wiki tatu baadaye.

Hata hivyo, Kocha Pep Guardiola anaamini atakuwa fiti kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki mmoja baadaye. Majeruhi hayo ya Ederson ina maana hataichezea timu yake ya taifa ya Brazil kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya England utakaofanyika uwanjani Wembley, Jumamosi.

Kutokana na kipa wa Liverpool, Alisson kuwa majeruhi, mechi hiyo ya England na ile ya Hispania wiki inayofuata, ilikuwa nafasi muhimu kwake kusimama kwenye goli la Brazil.

Lakini, kocha Guardiola amekuwa na imani kubwa na kipa wake namba mbili, Stefan Ortega, ambaye alionyesha kiwango bora alipoingia kuchukua nafasi ya majeruhi Ederson uwanjani Anfield.

Kipa Ortega mpango wake ni kuwa namba moja kwenye kikosi hicho cha Etihad na lisemwalo ni yupo kwenye mazungumzo ya kufahamu hatima yake kabla ya msimu huu kufika tamati.

Chanzo: Mwanaspoti