Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ederson akiondoka, Ortega anachukua namba

Ederson X Ortega Ederson akiondoka, Ortega anachukua namba

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ripoti za kuhusu kuondoka kwa kipa namba moja wa Manchester City, Ederson zimezidi kupamba moto, wakati Mbrazili huyo akihusishwa na klabu za Saudi Arabia zinazohitaji huduma yake kwenye dirisha hili.

Mwishoni mwa msimu wa 2023-24, Ederson aliripotiwa kuwa kwenye rada za klabu za Saudi Pro League, lakini hakuna timu hata moja iliyopeleka ofa rasmi huko Man City kwa ajili ya kuhitaji huduma ya mchezaji huyo.

Lakini, miamba hiyo ya Etihad, ambayo msimu uliomaliza ilibeba taji lao la nne mfululizo la Ligi Kuu England imeshaanza maandalizi endapo kama itampoteza Ederson kwenye dirisha hili baada ya kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja kipa Stefan Ortega, ambaye anatazamiwa kwenda kuwa namba moja msimu ujao.

Gazeti la The Independent limeandika: "Stefan Ortega ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na Manchester City ambao utampa nafasi ya kutumika kama kipa chaguo la kwanza hadi 2026.

"Ederson bado anatajwa kuwa mlengwa mkuu katika klabu za Saudi Arabia, lakini hadi sasa hajaomba kuondoka na Man City haijapokea ofa yoyote kwa ajili yake."

Chanzo: Mwanaspoti