Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ederson afunguka

Ederson X Ortega Ederson afunguka

Sun, 28 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa Manchester City, Ederson, 30, amesema taarifa zinazodai kwamba anamuonea wivu kipa mwenzake Stefan Ortega juu ya kiwango alichoonyesha katika mechi za mwisho wa msimu uliopita zilizoamua ubingwa sio za kweli, pia amesisitiza kwamba anawaza jinsi ya kuisaidia timu msimu ujao licha ya tetesi zinazodai kwamba anaondoka.

Kipa huyu wa kimataifa wa Brazil amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Pep Guardiola kilichoshinda mataji manne mfululizo ya Ligi Kuu England.

Ederson ambaye alisajiliwa kwa Pauni 33 milioni mwaka 2017 kuchukua nafasi ya Claudio Bravo, anatajwa kama mmoja kati ya makipa bora zaidi duniani linapokuja suala la kuchezea mpira kwa kutumia miguu na mara kadhaa amekuwa akifananishwa na kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer.

Taarifa zilizoripotiwa na The Athletic mapema wiki hii zilieleza kwamba Ederson ‘alikwazika’ na sifa alizokuwa anapewa kipa mwenzake Ortega kwa kusimama vyema katika lango baada ya kuingia akitokea benchini kwenye mchezo dhidi ya Tottenham msimu uliopita ambapo aliokoa shambulizi matata lililofanywa na Son Heung-min.

Baada ya taarifa hiyo, Ederson ambaye anahusihwa na Al Ittihad ya Saudi Arabia aliandika katika ukurasa wake wa Instagram kukanusha hilo.

“Ningependa kufafanua kwamba habari iliyochapishwa na The Athletic, inayosema kwamba sikupendezwa na kucheza kwa kipa mwenzangu (Ortega), sio za kweli, siku hiyo walioripoti ilikuwa ni moja kati ya siku ngumu sana katika maisha yangu ya soka, kwa sababu nilipata jaraha lililonizuia kucheza katika kipindi chote cha mwisho cha msimu na hata kuiwakilisha nchi yangu katika michuano ya Copa America,” alisema Ederson na kuongeza:

“Nilipoumia katika mchezo huo, mawazo yangu ilikuwa ni kuendelea tu kucheza ili kuisaidia timu katika harakati za kutetea taji, lakini majeraha niliyopata yalikuwa makubwa na nisingeweza kucheza ingawa akili ilikuwa inatamani.”

Chanzo: Mwanaspoti