Eden Hazard bado anaweza kuwashangaza watu kwa uhamisho anaoweza kuufanya siku zijazo kutokana na ahadi ambayo inasemekana alitoa mapema mwanzo wa soka lake la kulipwa.
Imekuwa ni changamoto kwa Hazard katika klabu ya Real Madrid, winga huyo ambaye anatatizika na shida ya majeraha na kuwa kwenye fomu nzuri tangu alipowasili 2019.
Mbelgiji huyo aliigharimu Real Madrid zaidi ya Euro milioni 100, lakini thamani yake bado haijathibitika Real. Anatarajiwa kusalia Santiago Bernabeu kwa siku zijazo, akidhamiria kujiimarisha zaidi.
Lakini kwa mujibu wa makamu wa rais wa Westerlo Hasan Cetinkaya, Hazard tayari ameahidi kuichezea klabu ya Fenerbahce ya Uturuki katika siku zijazo.
“Naamini ninaweza kumchukulia Eden Hazard kama rafiki. Nimemfahamu tangu nikiwa Lille na aliniahidi kuwa siku moja ataichezea Fenerbahce. Westerlo itakuwa ngumu zaidi, lakini huwezi kujua. Labda atamalizia kazi yake hapa.” – Hasan Cetinkaya,
Bila shaka staa huyu hajapanga kuelekea Uturuki katika kipindi hiki, huenda akafanya hivyo katika hatua zaker za mwisho za maisha yake ya soka la kulipwa. Kuna tetesi kuwa kwa sasa anatarajia kurejea EPL.
Vilabu vya juu vya Uturuki vinalipa vizuri, na kama vile Fenerbahce na Galatasaray wana baadhi ya mashabiki wenye mapenzi makubwa barani Ulaya.