Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eden Hazard bado yupo sana Real Madrid

Eden Hazard.jpeg Eden Hazard

Sun, 15 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Safari ya Eden Hazard kuondoka Uingereza kama staa anayetegemewa zaidi hadi kuwa nyota anayetupiwa lawama zaidi Real Madrid, inaweza kuwa kuonekana kama hadithi, lakini ndiyo uhalisia.

Staa huyu amekumbwa na majeraha sana tangu kuwasili Real Madrid, kiasi cha kushindwa kutoa mchango uliofikia matarajio ya mashabiki wengi wa Real Madrid na wapenzi wengine wa soka.

Staa huyu aliyeonekana kupoteza ladha na kushuka kiwango ukifananisha na alipokuwa EPL, amekuwa akihusishwa na kuondoka klabuni hapo, huku vilabu kadhaa vikitajwa kuhitaji huduma yake.

Hata hivyo, bosi wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amebainisha kuwa staa huyu atasalia klabuni hapo.

“Mpango wake uko wazi kabisa. Anasalia na anafanya hivyo akiwa na motisha kwa kuwa amekuwa na wakati mgumu kwa miaka hii ya mwisho. Anataka kuonesha ubora wake.” – Carlo Ancelotti akimzungumzia Eden Hazard

Chanzo: www.tanzaniaweb.live