Uongozi wa Klabu ya Newcastle United umemtangaza Eddie Howe, kuwa mbadala wa Kocha Steve Bruce ambaye alifutwa kazi klabuni hapo mwezi uliopita, baada ya mfululizo wa matokeo mabaya katika viunga vya St. James Park jijini Tyne.
Howe alikuwa mapumzikoni baada ya kuondoka Bournemouth 2020 aliposhuka daraja na sasa anarejea kwenye majukumu mapya akiwa na timu mpya ambayo ina hesabu kali yakuwa miongoni mwa Vilabu tishio barani Ulaya.
Newcastle awali walikuwa wanatajwa kumchukua kocha wa zamani wa Arsenal ambaye kwa sasa anainoa Villarreal Unai Emery ila alichagua kubaki ndani ya La Liga, jambo ambalo limewafanya matajiri hao wasiwe na chaguo juu yake.
Rekodi zinaonyesha kuwa Howe katika kazi ya ukocha amesimamia jumla ya mechi 545, ameshinda mechi 228, sare 114 na vichapo vya idadi ya mechi 203.
Howe amesema kuwa ni jambo kubwa kwake kuweza kuwa kocha kwenye timu hiyo hata familia yake inafurahi kushusu hilo.
“Ni heshima kubwa kuja kuwa kocha hapa kwenye timu yenye historia kama Newcastle United, ni siku kubwa kwangu na familia pia” amesema Howe,ambaye leo Jumanne atafanya mazoezi na timu hiyo kwa mara ya kwanza.