Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ecuador hatarini kuondolewa kombe la Dunia

Ecuador Ecuador

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ecuador ipo hatarini kuondolewa katika Kombe la Dunia 2022 kutokana na utata wa nyaraka za mchezaji wao, Byron Castillo, ikiwemo hati ya kusafiria ambapo inadaiwa beki huyo ni raia wa Colombia.

Uchunguzi wa awali umebaini kuna cheti cha kuzaliwa kinachoonesha Castillo alizaliwa Colombia, lakini inavyoonekana aliingia Ecuador kinyemela kutafuta maisha, baadaye Shirikisho la Soka la Ecuador (FEF) likashiriki kumtengenezea nyaraka za uwongo ili kuthibitisha Uraia wake.

Kamati ya Rufaa ya #FIFA inatarajiwa kukutana Septemba 15, 2022 kujadili suala hilo ambapo beki huyo alichezea mechi 8 za kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live