Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ecuador, Uruguay zafuzu Kombe la Dunia 2022

Uruguay Ecuador, Uruguay zafuzu Kombe la Dunia 2022

Sat, 26 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu za taifa za Uruguay na Ecuador zimefanikiwa kukata tiketi ya kwenda Qatar ambako fainali za michuano ya kombe la Dunia zimepangwa kufayika mwezi Novemba mpaka Disemba mwaka huu.

Ecuador licha ya kufungwa na Paraguay kwa mabao 3-1 lakini wamefuzu kushiriki kombe la Dunia wakinufaika na ushindi wa Uruguay ambao waliifunga Peru 1-0 bao lililofungwa na G.D Arrascaeta kipindi cha kwanza cha mchezo.

Ecuador walishindwa kufuzu kombe la Dunia la mwaka 2018 ambalo lilifanyika Russia walikuwa wanahitaji alama moja pekee kujihakikishia nne za juu.

Peru bado wanashikiria hatima yao ya mchujo, ingawa Colombia na Chile zinaweza kuwapata wakati Paraguay tayari imetolewa kwenye nafasi ya kufuzu wanasubiri mechi ya mwisho Jumanne mjini Lima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live