Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EURO 2024: Mashabiki wachapana baa

Mashabiki Wazichapa EURO 2024: Mashabiki wachapana baa

Fri, 14 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Euro 2024, kati ya wenyeji Ujerumani dhidi ya Scottland, taarifa zinadai mashabiki wa timu hizo mbili walipigana Jumatano ya wiki hii.

Jiji la Munich linadaiwa kuwa bize kwa sasa baada ya mashabiki wengi kuwasili kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa ufunguzi na taarifa kutoka Daily Record zimefichua watu wawili walilishambulia kundi la mashabiki wa Scottland katika baa moja maeneo ya Marienplatz, Munich.

Mzozo huo ulianza baina ya watu wawili ambao wanadaiwa ni mashabiki wa Ujerumani na kundi la mashabiki wa Scottland kisha wawili hao wakaondoka.

Baada ya muda wakarejea na kuanza kuwarushia viti mashabiki wa Scottland na kama haitoshi walichukua glasi za pombe na kuanza kuwapiga nazo, hali iliyozua mzozo kwani wale wa Scottland nao walirudisha mapigo.

Hata hivyo, hakukuwa na mtu yeyote aliyepata majeraha katika tukio hilo na baada ya muda polisi waliwasili eneo hilo na wakawakamata watu hao wawili na baadhi ya mashabiki wa Scottland.

Tukio hilo linadaiwa kutokea mida ya saa 3:30 usiku kwa saa za huko.

Inaelezwa kunaweza kuwa na vurugu zaidi ya hizo viwanjani na sehemu za starehe huku mashabiki wa Serbia wakionekana kuwa ndio watakuwa tatizo kubwa kutokana na historia yao wanapoenda kwenye mashindano mbalimbali.

Chanzo: Mwanaspoti