Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EPL kupitia maamuzi ya VAR

VAR PREMIER LEAGUE EPL kupitia maamuzi ya VAR

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi kuu ya uingereza ‘Premier League’ watapitia maamuzi tata yaliotolewa na VAR kwenye mchezo kati ya west ham na Newcastle ya wikiendi hii ambayo yalipelekea kukataliwa kwa magoli kama jambo la ‘kipaumbele’ kwenye bodi ya waamuzi PGMOL.

Newcastle walikataliwa goli lao dhidi ya Crystal Palace, wakati West Ham walishuhudia goli lao la kusawazisha dhidi ya Chelsea kwenye dimba la Stamford Bridge likikataliwa.

Magoli yote yalikataliwa baada ya mapitio ya maamuzi ya VAR, baada mwamuzi kuombwa kwenda kuomba ushauri kwa waamuzi wa nje ya uwanja kupitia Tv na kupindua matokea halisi.

Newcastle walimaliza mchezo kwa sare ya kutokufangana na Crystal Palace wakati West Ham walipoteza kwa matokeo ya 2-1 dhidi ya Chelsea, huku kocha David Moyes na Kapteni Declan Rice wakiongoza kukosoa maamuzi hayo.

Rice alinukuliwa akisema: “Hiyo ilikuwa moja ya maamuzi mabovu ya VAR tangu kuanzushwa kwake kwenye mchezo huu.” Wakati David Moye alienda mbali zaidi kwa kuita “Kashfa” maamuzi baada ya kuleta sintofahamu uwanjani na kupelekea malalamiko kwa mwamuzi.

“Ni maamuzi ya kashfa.” Alisema Moyes. “Mwamuzi alishatoa maamuzi na sijui nani alimtuma kwenda VAR lakini nilifikili atasema goli mara tu ya kwenda kwenya kwenye Tv.

Nimeangalia kwa kona zote na ilikua ngumu sana kuona na kwa jinsi gani amelikataa. Sijui ni nani yupo VAR aliyemtuma kule. Kitu kibaya ni uwezo wa waamuzi wetu bora kwa kipindi hiki.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live