Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EPL kupigwa Krismasi baada ya miaka 28

Chelsea Vs Wolves EPL kupigwa Krismasi baada ya miaka 28

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mechi za Ligi Kuu England (EPL) zitaanza tena kuchezwa siku ya Krismasi mwaka huu kufuatia uamuzi wa kurudisha utaratibu huo ambao mara ya mwisho ulitumika mwaka 1995, uliofanywa na bodi ya Ligi hiyo juzi Ijumaa.

Na kwa kuanzia, mechi ya kwanza itakayoshuhudiwa kuchezwa siku ya Krismasi baada ya miaka 28 kupita bila jambo hilo kufanyika, utakuwa ni ule wa Wolves dhidi ya Chelsea ambao awali ulipangwa kuchezwa Disemba 23.

Sababu ya kurudisha utaratibu huo wa kucheza mechi siku ya sikukuu ya Krismasi ni kutimiza matakwa ya mdhamini wa haki za matangazo ya luninga wa ligi hiyo na baada ya hapo, utaendelea miaka ijayo.

Baada ya mwaka 1995, mechi za EPL hazikuwa zinachezwa siku ya sikukuu ya Krismasi na badala yake zilikuwa zinafanyika ama siku moja au mbili kabla au siku moja baada kwa maana siku ya sikukuu ya Boxing Day.

Hata hivyo uamuzi huo unaonekana kutofurahiwa na klabu nyingi ambazo zinadai hauwatendei haki mashabiki wao ambao siku hiyo huwa wanaitumia kujumuika pamoja na kusherehekea badala ya kwenda viwanjani.

"Uamuzi huu haukubaliki kabisa na ni sawa na kupiga vibao usoni mashabiki wa dhati wa soka. Katika kipindi ambacho tunahangaika kusaidia mashabiki kusafiri kwenda mechi za ugenini, inachanganya kuona kihunzi kingine kinawekwa kwenye njia yao," alisema mwenyekiti wa Chama cha Mashabiki wa Chelsea, Mark Meehan.

Chanzo: Mwanaspoti