Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EPL imenoga, City yaweka ubingwa rehani

Riyad Mahrez Sad Winga wa Man City, Riyad Mahrez akisikitika

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester City imekosa fursa ya kuweka pengo la alama sita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kubanwa mbavu na Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Selhurst Park.

Licha ya City kutawala mchezo kwa muda mrefu walishindwa kuifungua ngome ya ulinzi ya Palace na kuishia kugonga mwamba mara mbili huku beki wa kati Aymeric Laporte akipoteza nafasi ya dhahabu ungwe ya kwanza.

Kwa matokeo hayo, Liverpool inaweza kupunguza pengo la pointi na kufikia moja endapo watashinda mchezo wao wa Jumatano dhidi ya Arsenal.

Kwa upande wa Crystal Palace matokeo hayo yanamaanisha wametengeneza mazingira ya kumaliza msimu kwenye kumi bora ingawa kwa sasa wanashika nafasi ya 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live