Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EPL: Yatangaza visa 103 Vipya vya Uviko-19

Gettyimages 1227635154 1024x576 EPL, Yatangaza visa 103 Vipya vya Uviko-19

Tue, 28 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

EPL imetangaza visa vipya 103 kwenye vilabu vyake, wakiwemo wachezaji na wasaidizi, ni kiwango cha juu kurekodiwa kwa wiki tokea walipoanza kufanya vipimo mwezi May mwaka jana.

Bodi ya ligi imethibitisha kwamba kuanzia Jumatatu 20 Disemba hadi Jumapili 26 Disemba, wachezaji na staff wa benchi 15,186 walipimwa na kati yao 103 walikutwa wana maambukizi mapya.

“Bodi ya ligi imeanza kuchukua hatua za kujikinga na uviko-19 kwa kuvaa barakoa, kukaa kwa umbali, kupunguza muda wa matibabu na pia kuongeza kasi ya upimaji, pia bodi inafanya kazi kwa pamoja na vilabu ili kuhakiksha usalama wa watu na kupunguza hatari ya kuenea kwa Uviko-19.

“Pia inashirikiana kwa karibu na serikali kuu, serikali za mitaa, taasisi na makundi mbalimbali ilikuweza kufuata mabadiliko yanayotolewa na miongozo kwa ustawi mzuri wa baadae.” Waraka wa bodi ya ligi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live