Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EPL Kurudisha Sub 5 Msimu Ujao

EPL SUB EPL Kurudisha Sub 5 Msimu Ujao

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miongoni mwa ligi kubwa barani Ulaya, ni EPL pekee ndio inaendelea na mfumo wa Sub 3 badala ya 5 ambazo zinatumika sehemu zingine. Mabadiliko yanakuja.

Kuelekea mwishoni mwa msimu, kunauwezekano vilabu vinavyoshiriki EPL vikapiga kura ya kuamua matumizi ya mabadiliko 5 au wabaki na mfumo wao wa sasa (3). Hii ni baada ya baadhi ya makocha na wachezaji kupaza sauti zao kwenye kutaka mabadiliko hayo.

Japokuwa kuna upinzani wa matumizi ya sub 5 (hasa kutoka katika vilabu vyenye wachezaji wachache), shirikisho la wachezaji nchini Uingereza linaunga mkono mabadiliko hayo wakiamini kuwa, lengo kubwa ni kuwalinda wachezaji na sio kuvibeba vilabu kwa namna yeyote.

Juni 2022 inatajwa kuwa ndio mwezi wa maamuzi wakati ambapo, vilabu vyote vya EPL vitakutana kwenye mkutano wa mwaka. Pamoja na mabadiliko ya sub, pia kuna suala la muda kati ya mchezo mmoja na mwingine. Pendekezo lililopomezani ni, kuwepo na tofauti ya walau saa 72 kati ya mchezo mmoja na mwingine ili kuwapa muda wachezaji kupumzika kabla ya mchezo mwingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live