Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dzeko: Tuongeze kasi kuwafikia Napoli

D9EB3230 18DF 44AA 80BA 95128C3CA98A.jpeg Edin Dzeko

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan ya nchini Italia raia wa Bosnia Edin Dzeko amesema klabu yake inaweza kuwafikia vinara Napoli ambao wanaongoza ligi kuu ya Italia.

Mshambuliaji huyo amekiri kuwa klabu yake ya Inter Milan inahitaji kuongeza kasi na kufanya kazi kubwa ili kuweza kuwafikia vijana wa Luiciano Spaletti vinara klabu ya Napoli ambao wamekua na msimu bora.

Klabu ya Inter Milan ambayo ilibeba ubingwa msimu mmoja uliopita kabla ya majirani zao klabu ya soka ya Ac Milan kubeba ubingwa msimu uliomalizika,Huku klabu hiyo ikiwa imeanza msimu huu vibaya baada ya kupoteza michezo mitano ya awali kati ya 15 waliyocheza kabla ya mapumziko ya Kombe la Dunia.

Mshambuliaji wa Edin Dzeko anaelewa ugumu ambao wako nao kurudisha ubora wao baada ya ligi kurejea mwezi Januari mwakani,Huku mshambuliaji huyo akisisitiza kua wanahitaji kufanya kazi ya ziada ili kuwafikia klabu ya Napoli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live