Paulo Dybala anakaribia kuikataa Chelsea huku akiwa tayari kuongeza kandarasi yake na AS Roma, licha ya Chelsea, Newcastle United na Saudi Arabia kumtaka.
Mkataba wa sasa wa Muargentina huyo utaendelea hadi Juni 2025, kukiwa na kipengele cha Euro milioni 12 cha kutolewa kwa timu zisizo za Italia. Hata hivyo, Dybala anaonekana kutosheka kubaki Stadio Olimpico akiwa na imani kubwa ya kuzidi kupata nafasi na kukuza karia yake ya mpira.
Hata hivyo makubaliano yamefikiwa kati ya Tiago Pinto na wawakilishi wa Dybala,pia wameboresha mkataba wake kwa nyongeza ya mishahara kutoka Euro milioni 4.5 pamoja na bonasi hadi Euro milioni 6. Nyongeza ya mkataba itakuwa halali hadi 2026, na Roma pia ina chaguo la kuongeza zaidi kwa msimu mwingine.
Chelsea imeweka bei ya pauni milioni 50 kwa Conor Gallagher kutoka kwa West Ham United kuhusu uwezekano wa uhamisho wa kiungo huyo. Wakati Tottenham nao wameonyesha nia, West Ham wamechukua uongozi na ombi lao la awali la pauni milioni 40 kukataliwa na Chelsea. The Hammers hawataki kuvuka ofa yao ya pauni milioni 37, na nyongeza ya pauni milioni 3, kama ilivyoripotiwa na Evening Standard.
Zaidi ya hayo, wakati Muingereza huyo amebakiza miaka miwili pekee kwenye mkataba wake, Sky Sports imeripoti kuwa Chelsea wako tayari kurefusha mkataba wake pia zaidi ya hayo, ripoti hiyo inasema Mauricio Pochettino amemjumuisha kiungo huyo katika mipango yake ya msimu ujao na kumuacha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuondoka.