Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dyabala kurejea Juventus kwa vipimo zaidi

Dyabala (600 X 401) Nyota wa Juventus, Paulo Dyabala

Tue, 16 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa juventus Paulo Dybala atakosekana kwenye mchezo wa kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Brazil kwa sababu ya matatizo ya misuli.

Dyabala alipata matatizo hayo ya msuli baada ya kugongana na mlinzi wa timu ya taifa ya Uruguay Joaquin Piquerez kwenye mguu wake wa kushoto kwenye mchezo wa kufuzu kombe la Dunia kati ya Uruguay na Argentina.

Paulo anatarajiwa kusafiri leo kurudi nchini Italia, ambapo kesho jioni atatua kwenye ardhi hiyo na kwenda moja kwa moja kufanyiwa vipimo, na kuangalia ukubwa wa jeraha ikiwa kama ataweza kujumuishwa kwenye mchezo unaofwata dhidi ya Lazio kwenye Serie A.

Pia klabu ya Juventus inatarajia kumpa mkataba mpya mshambuliaji huyo mwezi huu, na mpaka sasa Dyabala ameichezea Juventus michezo tisa kwenye msimu huu ndani ya Serie A.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live