Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dyabala kulikosa Kombe la Dunia Qatar

B1FC7C56 D4CE 49F9 A625 CA5ED45092C0.jpeg Paul Dyabala kulikosa kombe la Dunia

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paulo Dybala anaweza kutoshiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar baada ya kupata jeraha la misuli alipokuwa akiicheza katika klabu yake ya Roma.

Mshambuliaji huyo wa Argentina alikuwa akichezea kikosi cha Jose Mourinho katika mchezo wao wa Serie A na Lecce alipoenda kupiga mkwaju wa penati.

Akiwa amesimama akiwa amejitengenezea mpira, Dybala alipiga penalti iliyompita kipa Wladimiro Falcone na kuwapa Roma uongozi wa 2-1 kwenye mechi hiyo, lakini mara moja akaonyesha dalili ya kutokuwa sawa katika msuli wake.

Wakati akielekea kushangilia, mshambuliaji huyo alionekana kuugulia kwa maumivu huku wachezaji wenzake wakiungana naye kabla ya madaktari kumshughulikia.

Dyabala mwenye umri wa miaka 28 akishika paja lake, alitolewa nje ya uwanja na nafasi yake ikachukuliwa na kiungo wa zamani wa Manchester United Nemanja Matic.

Fowadi huyo alionekana kuwa na uhakika wa kuchezea Argentina katika michuano ijayo ya Kombe la Dunia itakayoanza mwezi ujao. Lakini, kwa mujibu wa bosi wa Roma Mourinho, inaonekana kwamba matumaini ya Dybala kupitishwa akiwa fiti ni finyu.

Mourinho alisema “Ninasema ni mbaya, bila kusema sana, mbaya sana. Kwa bahati mbaya, ni mbaya zaidi kuliko [tu] mbaya.”

Alipoulizwa kama Dybala anaweza kurejea kabla ya mwisho wa mwaka, Mourinho aliongeza: “Mimi si daktari na sijazungumza na mmoja, lakini kutokana na uzoefu wangu, kutokana na kile nilichoelewa nilipozungumza na Paulo, [itakuwa] magumu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live