Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duncan apewa kazi maalumu

Dancar Nyoni Pic Data Duncan Nyoni

Sun, 24 Oct 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Katika kuhakikisha Jwaneng Galaxy ya Botswana inapasuka mapema Kwa Mkapa, Kocha Didier Gomes ameonekana akimpa kazi maalumu winga wake mpya Duncan Nyoni mazoezini na Mmalawi huyo hakumuangusha.

Duncan aliyesajiliwa hivi karibuni, alipewa kazi ya kupiga friikikii, huku timu nzima ikipewa mbinu za kukaba na kushambulia kwa pamoja kuonyesha kuwa kesho Wabotswana watakuwa na kazi kubwa kwa Wekundu wa Msimbazi hao.

Mwanaspoti lililokuwepo mazoezi ya Simba yanayoendelea Uwanja wa Boko Veterani, lilishuhudia baada ya programu za kukaba na kushambulia kumalizika, Gomes aliwaita Duncan, Bernard Morrison, Rally Bwalya, Erasto Nyoni, Israel Mwenda, Mohamed Hussein na Thadeo Lwanga na kuanza kuwapa somo namna ya kupiga frii kiki.

Walisogea katika moja ya goli la uwanja ule na kupanga midoli iliyosimikwa kama watu walioweka ukuta, langoni akiwepo Ally Salum kisha kuanza kupiga kwa kupokezana na aliyeshindwa mara nyingi alitoka na hatimaye kubaki Bwalya na Duncan.

Wawili hao walionyesha ubora zaidi huku Duncan akifunika kwa kufunga frii-kiki zile akitupia kambani zaidi ya mara tano na baada ya hapo Mwanaspoti lilizungumza na Gomes ambaye alimsifu Duncan katika kupiga frii-kiki.

“Ni mtaalamu sana, anajua ni upande gani atapiga na nguvu gani ataweka mguuni ili kufunga. Nadhani atatusaidia sana katika hili kama tutapata frii-kiki akiwa uwanjani,” amesema Gomes na kuongeza;

“Baada ya kuondoka kwa Chama (Clatous) na Luis (Miquissone) ambao mara nyingi walikuwa wakipiga frii-kiki nadhani sasa atakuwa anapiga Duncan na kina Bwalya, Israel na Morrison.”

Chanzo: Mwanaspoti