Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duke Abuya afunguka siri ya ubora wake dhidi ya Augsburg

Duke Abuya Mzz.jpeg Duke Abuya afunguka siri ya ubora wake dhidi ya Augsburg

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mpya wa Klabu ya Yanga, Duke Abuya raia wa Kenya, amefunguka siri ya kuonesha kiwango bora katika mchezo dhidi ya FC Augsburg tuliocheza Uwanja wa Mbombela nchini Afrika Kusini.

Abuya aliyeingia kipindi cha pili akitokea benchi, amewavutia Wananchi kwa namna alivyocheza dhidi ya Wajerumani hao licha ya mchezo huo kupoteza kwa magoli 2-1.

“Tunamshukuru Mungu mchezo umemalizika salama. Tuna timu nzuri kulingana na tunavyocheza ni rahisi kushirikiana.

“Kuna maelekezo mwalimu alinipatia nashukuru nilifuata na kila kitu kimekuwa vizuri. Nashukuru Mungu naomba niendelee kucheza hivi. Nashukuru sana kwa Wananchi pia waendelee kutusapoti kila kitu kitakuwa vizuri.

“Kucheza na wachezaji wenye viwango vya juu inakuwa sio ngumu sana, unapambana nao na inasaidia, nashukuru pia wachezaji walio karibu yangu ni wazuri inakuwa rahisi sana,” alisema Abuya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live