Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duh Simba kumbe wachovu tu kwa wababe Ligi Kuu

Simba SC VVV Simba SC

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa sare ya bao 1-1 dhidi Singida Big Stars, Simba imeshindwa kubeba pointi tatu mbele ya vigogo wakubwa waliowekeza fedha nyingi msimu na wanaowania nao ubingwa wa Ligi Kuu kwa karibu zaidi.

Simba ilitoka sare ya bao 1-1 na Yanga na ikafungwa bao 1-0 na Azam Fc. Singida juzi ilishindwa kutamba kwenye uwanja wake wa nyumbani Liti mkoani hapa ikiwa na mziki wake wote.

Singida ndiyo ilianza kupata bao dakika ya 11 likifungwa na staa wa zamani wa Yanga, Deus Kaseke akimalizia krosi ya kiungo Said Ndemla na kuunganisha mpira huo na kumpoteza kipa wa Simba Beno Kakolanya. Kaseke anakuwa mzawa wa kwanza msimu huu kuifungia bao Singida Big Stars kwani katika mabao yote tisa waliyofunga manane wamefunga wageni.

Hii ni sare ya tatu msimu huu kwa Singida Big Stars ya Kocha Hans Pluijm baada ya suluhu na Dodoma Jiji Septemba 11 kisha kufungana bao 1-1 dhidi ya Geita Gold Septemba 21.

Kwa upande wa Simba hii nayo ni sare ya tatu msimu huu baada ya kufungana 2-2 na KMC Septemba 7 kisha 1-1 na Yanga Oktoba 23.

Kinara wa mabao wa Simba, Mzambia Moses Phiri alishindwa kumalizia krosi ya Shomary Kapombe dakika ya nane tu tangu kuanza kwa mchezo huo akiwa yeye na kipa Khomeny Abubakary ambapo alipiga mpira uliotoka nje.

Singida waliipeleka Simba mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0 kabla ya kipindi cha pili kusawazisha bao hilo kupitia Peter Banda dakika ya 58.

Kwa matokeo hayo timu hizo zote zina pointi sawa 18, zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa ambapo Simba inashika nafasi ya pili huku Singida wakiwa nafasi ya tatu.

Kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko ambapo Kocha Juma Mgunda alimtoa Jonas Mkude nafasi yake ikichukuliwa na Banda.

Mabadiliko hayo yaliyofanyika dakika ya 46 yaliisaidia Simba kuongeza nguvu ambapo mshambuliaji wao Kibu Denis nusura aipatie bao timu yake lakini shuti lake liliokolewa na Khomeny.

VIKOSI

Singida Big Stars: Abubakary Khomeny, Paul Godfrey, Shafiq Batambuzi, Abdulmajid Mangalo, Carno Biemes, Bruno Gomes, Dario Frederico, Deus Kaseke, Said Ndemla Peterson Cruz, Meddie Kagere na Rodrigues Figuiredo

SIMBA: Beno Kakolanya, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Henock Inonga, Jonas Mkude, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, Kibu Denis, Moses Phiri Pape Sakho.

Kocha wa Simba, Juma Mgunda alisema makosa ambayo yalijitokeza kwenye kikosi chake wataenda kuyafanyia kazi ili kuwa bora zaidi kwenye michezo inayofuata,”Vijana walipambana lakini ndio mpira, yapo ambayo tumeyaona kama benchi la ufundi hivyo tutaenda kuyafanyia kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live