Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duh! Rooney amfanyia kitu kibaya Moyes

Rooney X Moyes Duh! Rooney amfanyia kitu kibaya Moyes

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wayne Rooney amefichua kwamba alimwagia ndoo nzima ya maji baridi kocha David Moyes wakati alipokuwa akijisaidia chooni.

Gwiji huyo wa England, Rooney aliibukia kwenye klabu ya Everton wakati huo ilipokuwa chini ya Moyes huko Goodison Park.

Moyes alihusika kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya kisoka ya Rooney, ambaye ndiye aliyempa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kwenye soka la timu ya wakubwa mwaka 2002 kipindi hicho alipokuwa na umri wa miaka 16 tu.

Lakini, hilo halikumfanya Rooney kuacha utukutu wake kwa kummwagia maji baridi kocha wake alipokwenda chooni wakati walipokuwa mazoezini.

Rooney alisema: “Hivyo bana, Moyes alipatwa na tumbo wakati tupo mazoezini, hivyo alikwenda chooni, alitumia vyoo vya timu ya kikosi cha kwanza kwa sababu ndio vilivyokuwa karibu. Aliingia chooni na kujifungia mlango. Nilijua alichokuwa akifanya huko na hapo, wachezaji wenzangu, wakaanza kuniangalia mimi. Niliona wanajaza ndoo maji baridi. Ni kama walikuwa wakisema, ‘Twende kazi.’ Nami ni kama nilikuwa nasema, ‘Leteni hiyo ndoo.’

“Nilienda chumba cha choo cha jirani yake na kumwaga maji kwenye choo alichokuwa Moyes kama vile nilikuwa naosha ndoo.”

Baada ya hapo, Rooney hakutaka kusubiri kuona nini kilimtokea kocha huyo baada ya kumwogesha maji baridi mwili mzima.

“Nilikimbia haraka sana kutoka kwenye eneo lile,” alisema Rooney. “Nilitoweka kwenye eneo hilo. Sikusubiri kuona nini kinatokea.”

Rooney aliondoka Everton mwaka 2004 kwenda kujiunga na Manchester United kabla ya kurudi tena huko Goodison Park baada ya zaidi ya miaka 13 ya kutamba kwenye kikosi cha Old Trafford.

Tukio hilo lilimfanya Moyes na Rooney kutokuwa na uhusiano mzuri, lakini baadaye walimaliza tofauti zao na maisha yanaendelea.

Chanzo: Mwanaspoti