Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duh! Ronaldo atishiwa Messi, Neymar anacheeeka

Ronaldo Mshs.jpeg Duh! Ronaldo atishiwa Messi, Neymar anacheeeka

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wamemwandama Cristiano Ronaldo kuwa kuipa nyimbo za Lionel Messi wakati mkali huyo wa Ureno timu yake ya Al Nassr ilipochapwa kwenye Kombe la Mfalme, huku Neymar akiangua kicheko jukwaani kwa kejeli hizo.

Ronaldo alishuhudia kikosi chake cha Al-Nassr kikichapwa kwa mikwaju ya penalti na Al-Hilal kwenye mchezo huo wa fainali ya Kombe la Mfalme. Mabao ya Aleksandr Mitrovic yalionekana kwamba yangeipa ubingwa wa mapema Al-Hilal kabla ya kipa David Ospina kuonyeshwa kadi nyekundu.

Ali Albulayhi naye alionyeshwa kadi nyekundu baada ya Ayman Yahya kuisawazishia Al-Nassr. Vurugu zilikuwa nyingi baada ya Kalidou Koulibaly naye kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Mechi hiyo iliingia kwenye hatua ya kupigiana penalti na hapo Al-Nassr ikakubali kichapo.

Jambo hilo lilimfanya Ronaldo kujiinamia na kumwaga machozi baada ya kuona siku zinakwenda tu bila ya ubingwa wowote.

Baadaye, mashabiki waliweka chumvi kwenye kidonda cha Ronaldo baada ya kuanza kuimba nyimbo za kumtukuza mpinzani wake wa muda mrefu, Messi, ambaye kwa sasa anacheza soka huko Marekani kwenye kikosi cha Inter Miami.

Neymar, ambaye anaichezea Al-Hilal hakucheza mechi hiyo kutokana na kuwa majeruhi, lakini alikuwa jukwaani na kuangua vicheko wakati mashabiki walivyokuwa wanamtesa Ronaldo kwa kuimba nyimbo za Messi, ambaye alicheza naye Barcelona na Paris Saint-Germain.

Ronaldo na Messi wamekuwa kwenye upinzani kwa muda mrefu wakati walipokuwa wanakipiga Hispania katika vikosi vya Real Madrid na Barcelona mtawalia. Na hilo linakuja ndani ya siku chache tu tangu mchezaji mwenzake wa zamani wa Ronaldo, Wayne Rooney, aliyewahi kucheza naye pamoja Man United, kudai kwamba Messi ni mchezaji bora kumzidi Mreno huyo.

“Nadhani Messi, yeye ndiye bora zaidi,” alisema Rooney.

Chanzo: Mwanaspoti