Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duh! Mipango ya Simba sio mtani kumbe

Simba Kimataifa April Wachezaji wa Simba wakimpongeza Shomari Kapombe

Mon, 18 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati tambo za pambano la Kariakoo Derby litakalochezwa Aprili 30 zikianza mtaani na mtandaoni kupitia mashabiki wa timu hizo, kwa mabosi wa Simba mambo ni tofauti, kwani wala hawashobokei pambano hilo kwa sasa.

Mabosi wa Simba wamesema kwa sasa akili zao zipo kwenye mechi zao za kimataifa za michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ili kumalizana kwanza na Orlando Pirates ya Afrika Kusini ndipo waanze kuifikiria Yanga.

Simba leo inatupa karata katika mechi ya mkondo wa kwanza ya robo fainali ya michuano hiyo ya CAF kabla ya kurudiana na wapinzani wao wiki ijayo ndipo itarudi kwenye Ligi Kuu Bara kuivaana na watani wao katika pambano hilo la derby.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mulamu Nghambi alisema

“Hatuwezi kufikiria mechi ya mbele zaidi kuliko iliyopo karibu, sisi tumejipanga kuhakikisha malengo yetu tuliyojiwekea ni kuwatoa wapinzani wetu na kufuzu hatua inayofuata,” alisema Mulamu na kuongeza;

“Baada ya hapo sasa tutaangalia kilichopo mbele yetu na ni maandalizi kwa ajili ya hao watani zetu huku tukiamini licha ya kutopoteza ila mechi yao ya kwanza kufungwa msimu huu watafungwa na Simba.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live