Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duh! Kumbe Xavi aliitosa Brazil

Xavi Hernandez Goal Xavi Hernandez

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Barcelona Xavi Hernandez amefichua kwamba alipewa nafasi ya kuinoa timu ya Taifa ya Brazil kabla ya Kombe la Dunia, lakini alikataa dili hilo na kujiunga na Barcelona.

Mchezaji huyo wa zamani wa Kimataifa wa Hispania alirithi mikoba ya Ronald Koeman mwaka jana akiwa kama kocha katika klabu hiyo yenye maskani yake Camp Nou.

Xavi amefichua kuwa alifuatwa na Rais wa Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) Rogerio Caboclo kuhusu jukumu la kuinoa Selecao wakati alipokuwa akiinoa Al Sadd, lakini akawakataa na kwenda Barcelona.

Xavi alisema kuwa; “Ilikuwa fursa iliyokuja kupitia kwa rais wa CBF, walikuja Qatar na kuzungumza na mimi na kuniuliza kama ningeweza kuwa sehemu ya wafanyakazi wa Tite, Lakini nilitaka kuwa kocha, sio msaidizi. Nia yangu ilikuwa kuwa kocha.”

Kocha huyo aliendelea kusema kuwa ingekuwa fursa nzuri sana ya kuweka historia, kuwa mzungu wa kwanza kufanya kazi katika timu ya Taifa ya Brazil, lakini wakati huo, haikutoke kwani alikuwa wazi kwamba alitaka kuwa kocha wa Barcelona ambayo ilikuwa ni ndoto yake na yuko pale.

Hata hivyo, Xavi alitania kwamba hatakataa kuchukua nafasi hiyo ikiwa itatolewa tena, na kuongeza: “Huwezi kujua. Itakuwa fursa ya kuvutia, lakini nia yangu ilikuwa kuchukua Barcelona, na huwezi kujua kuhusu siku zijazo ingawa ninafanya kazi kwa bidii, na huwezi kukataa chochote.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live