Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duh! Kisiga asema Simba ni Chama tu

Shaban Kisiga Marlow Kiungo wa zamani wa Simba, Shaban Kisiga

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa zamani wa Simba, Shaban Kisiga ameitazama timu hiyo, akasema anaiona nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza bila wasiwasi. Kwake mtu spesho ni Clatous Chama, ila wengine waliobakia watasubiri benchi kwake.

Katika nafasi anayocheza Kisiga ndani ya Simba yupo Chama aliyekiri anawajibika ipasavyo kwenye majukumu na ndio maana anatoa asisti za kutosha na anajiongeza kufunga anapoona ana nafasi hiyo, wengine ni Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin.

Alisema kwamba anawaheshimu wachezaji wote, lakini akataja sababu ya kujiamini kupata nafasi, kwamba anapenda kuwatuma washambuliaji kwenda mbele jukumu analoliona anayejitahidi kulifanya ni Chama, wengine wanawaza kufunga zaidi.

Alisema katika timu kila mmoja akifanya jukumu lake kikamilifu, inakuwa ngumu kutoa nafasi kwa mpinzani kupata matokeo kirahisi, akisisitiza kwa upande wake anapenda kutoa asisti zaidi kuliko kufunga.

“Kabla Chama hajaenda Morocco ndiye mchezaji aliyekuwa anaongoza kwa asisti Ligi Kuu Bara unajua kwa nini? anasimama kwenye majukumu yake, hana tamaa ya kutaka kufanya kila kitu mwenyewe,anawajibika kuliko mtu mwingine,”alisema Kisiga ambaye aliwahi kukipiga Simba, Mtibwa, Azam na Ruvu Shooting kwa nyakati tofauti.

Aliongeza;”Ukichunguza vizuri mastraika wengi wanapata taabu ya kusaka mipira na inakuwa rahisi kukabwa na mabeki, lakini kama viungo watawatuma mbele watafanya kazi yao vizuri, ndio maana nasema mimi sipendi sana kufunga kwa maana napenda kutengeneza nafasi zaidi kwa wengine.

“Nasisitiza na kulifafanua vizuri hilo, sina maana kwamba nikikaa kwenye nafasi ya kufunga na straika akawa amekabwa ama yupo mbali nitaacha, ila natamani kila mmoja awajibike kuziba njia,”anasisitiza staa huyo aliyeng’ara na Simba mwanzoni mwa miaka ya 2000 akitokea SC Villa ya Uganda.

Alisema soka linahitaji kutunza mwili, nidhamu na mazoezi vitu ambavyo anavifanya hadi sasa, hivyo haoni cha kumsumbua endapo akipata nafasi Simba na anaona kabisa anaweza akaisaidia kuongeza nguvu dhidi ya waliopo.

“Shida ya mashabiki wanamchoka mchezaji, ila nakwambia ukweli kuna wachezaji wa kigeni ni watu wazima kuliko sisi na wapo ndani ya vikosi hivyo na wanafanya kazi ya kawaida sana,” alisema Kisiga.

Timu ya mwisho aliyokuwa ameichezea Kisiga ni Mbeya City msimu wa 2021/22 na sasa yupo mtaani anasubiri mchongo kupitia usajili wa dirisha dogo.

“Kulikuwa na changamoto za hapa na pale ndio maana sikuendelea Mbeya City, pia kocha wa Prisons alinihitaji lakini mambo yakaenda ndivyo sivyo, sina shaka dirisha dogo nitarejea kwenye majukumu yangu,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live