Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duh! Kariakoo Dabi imechezwa dakika 74 tu

Yanga Vs Simba 20 April Duh! Kariakoo Dabi imechezwa dakika 74 tu

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Yanga wanaendelea na furaha ya ushindi wao walioupata juzi wa mabao 2-1 dhidi ya watani zao Simba ila moja ya jambo unalotakiwa kulifahamu ni mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa ulichezwa kwa dakika 74 tu.

Katika kipindi cha kwanza zilipoteza dakika 10 na kuufanya mchezo huo kuchezwa kwa dakika 35 huku kile cha pili zikiwa ni 39.

Mchezo huo uliokuwa ni wa kisasi kwa Simba hasa baada ya mechi ya mzunguko wa kwanza kupigwa mabao 5-1, Novemba 5, mwaka jana, ulionekana dakika nyingi zikipotea kipindi cha kwanza baada ya beki wa Simba, Henock Inonga kupata majeraha.

Beki huyo aliyeumia dakika ya 12 ya mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Kazi aliyesababisha penalti ya bao la kwanza kwa Yanga iliyopigwa na Stephane Aziz Ki dakika ya 20, mechi hiyo ilisimama dakika tatu wakati akipewa matibabu.

Dakika nyingine iliyopotea ni ya beki wa Yanga, Joyce Lomalisa kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Nickson Kibabage na mchezo ulisimama kwa dakika tatu huku nyingine 10 zilizobakia zikiwa ni kwenye mabadiliko ya wachezaji uwanjani.

Licha ya kupotea dakika 10 za kipindi cha kwanza ila ziliongezwa tatu na mwamuzi wa akiba, Tatu Malogo wa Tanga kama ilivyokuwa pia kipindi cha pili na licha ya kupotea sita aliongeza tano ambazo pia hakuweza kuzibalansi uwanjani.

Ushindi huo uliifanya Yanga kuendeleza rekodi yake bora pindi inapocheza na Simba Jumamosi kwani huo ulikuwa ni mchezo wa 61, kwao kukutana Ligi Kuu Bara tangu 1965 na imeshinda 26, kupoteza 16 huku 19 ikiisha kwa sare.

Yanga imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwani imefikisha jumla ya pointi 58 na kusalia kileleni baada ya kuchezo michezo 22 huku kwa upande wa Simba ikiwa ya tatu na pointi 46 baada ya michezo 21.

Ushindi huo wa Yanga umeifanya sasa kuhitaji pointi 16 tu katika michezo nane iliyosaliwa nayo ili kutangaza ubingwa mapema, kwani itafikisha jumla ya pointi 74 ambazo hazitaweza kufikia na Azam iliyopo nafasi ya pili kwa sasa ikiwa na alama 51 kwani hata ikishinda mechi zote nane ilizonazo (ukiwamo wa jana) itafikisha pointi 72 tu, wakati Simba ikishinda michezo tisa iliyosaliwa nayo itakuwa na uwezo wa kufikisha pointi 73 tu.

Yanga imesaliwa na mechi dhidi ya JKT Tanzania unaopigwa kesho Jumanne, Coastal Union, Mashujaa, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Dodoma Jiji, Tabora United na Tanzania Prisons, huku mechi nne zitakuwa na nyumbani na nne pia zitakuwa za ugenini, huku Simba ikiwa na mechi tano za nyumbani na nne za ugenini.

Mechi ilizosaliwa nazo Simba ni pamoja na ile ya kesho Jumanne utakaopigwa jijini Dodoma dhidi ya Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar ambazo zote ni viporo.

Pia wana mechi dhidi ya Namungo, Tabora Utd, Azam FC, Kagera Sugar, Geita Gold, KMC na JKT Tanzania.

Chanzo: Mwanaspoti